OFISA Habari wa Simba Haji Manara ameipongeza Serikali kwa kutoa ukomo wa mashabiki waakaohudhuria uwanjani kbaada ya taarifa ya awali kueleza kuwa watahitajika mashabiki 10 kwa kila timu.

Haji Manara amesema:"Serikali yetu ni sikivu, inashaurika na inakubali ile dhana ya kukosoana, baadhi ya watu mitandaoni walinilaumu kwa ushauri wangu huu, lakini leo taarifa iliyosainiwa na mawaziri wenye dhamana ya michezo na afya nchini wamesaini tamko lenye kuafiki uwepo wa mashabiki viwanjani ambapo sasa watalazimika kukaa umbali wa mita moja moja.

Kinachofurahisha tamko lao limeenda mbali zaidi na kuelezea jinsi mashabiki wanavyopaswa kuchukua tahadhari, sambamba na wachezaji pamoja na Viongozi.


Hii ndio Serekali sikivu tunayoizungumza, Serikali inayokubali kushauriwa na watu wa kawaida.


Hongera Waziri Harrison Mwakyembe kwa kukubali kuondoa ukomo wa mashabiki kumi viwanjani na hongera pia Waziri Ummy Mwalimu (Waziri wa Wizara ya Afya) kwa namna unavyoliongoza taifa katika mapambano hatari ya ugonjwa huu wa Covid 19.


Sasa ni wajibu wetu Mashabiki tutakaokwenda viwanjani kuzingatia masharti hayo ya kitaalamu ili nchi yetu iendelee kuwa salama zaidi.

Mwisho pongezi kwa Shirikisho letu la Soka nchini TFF chini ya Rais wetu shupavu Wallace Karia na Mtendaji mkuu wake mahiri 'Magician' Wilfred Kidao  kwa uongozi wao wenye maono na uliojaa busara nyingi, Mungu azidi kuwapa hekma ili waipeleke mbele zaidi nchi hii katika mchezo huu murua zaidi duniani. 🙏🏾🙏🏾🙏🏾

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.