JUMA Mgunda, Kocha Mkuu wa Coastal Union amesema kuwa kikosi chake kitarejea mazoezini hivi karibuni mara baada ya sikukuu ya Eid El Fitri kumalizika.
Juni Mosi, Ligi Kuu Bara ambayo ilisimamishwa na Serikali Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ambavyo vimeivuruga dunia inatarajiwa kurejea.
Mgunda amesema:"Tupo tayari kwa ajili ya ligi na tunatarajia kuanza mazoezi hivi karibuni mara baada ya sikukuu kupita kwani ni muhimu kufanya maandalizi.
"Pia tunatambua kuwa bado tunatakiwa kuchukua tahadhari hivyo kitakachofanyika ni kuendelea kufuata taratibu zilizowekwa na Wizara ya afya pamoja na Serikali ili kuwa salama."
Mgunda ni kocha Mzawa ambaye alimpa tabu Arstica Cioaba raia wa Romania kwa kumpiga nje ndani ambapo mechi ya kwanza ilikamilika kwa Azam FC kufungwa bao 1-0 na ile ya pili Azam ilichapwa mabao 2-1.

Post a Comment