UONGOZI wa Singida United umesema kuwa umebakiza dakika 810 za moto zitakazotoa hatma yao ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na mwendo wao kuwa wa kusuasua.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana alisema kuwa kurejea kwa ligi ni ishara ya wao kurejea vitani kumaliza kazi yao waliyoianza.

“Tuna mechi tisa mkononi ambazo zimebaki hizo zote ni mwendo wa kufa na kupona kwani tuna kazi kubwa ya kufanya  ili kubaki ndani ya ligi ukizingatia kwamba ushindani ni mkubwa.

“Mpango mkubwa ni kuona kwamba kila mechi tunacheza mithili ya fainali itakuwa njia pekee ya kutufanya tubaki msimu ujao kwa sasa tunaanza maandalizi ili kurejea vizuri,” alisema Katemana.

Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa na pointi 15 baada ya kucheza mechi 29 ikiwa imepokea vichapo mechi 20

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.