IMEELEZWA kuwa uongozi wa Simba upo kwenye mkakati kabambe wa kuboresha masuala ya utoaji wa taarifa kwa mashabiki wake jambo ambalo wameamua kuwashtua leo ifikapo saa saba.
Habari kutoka ndani ya Simba zinaeleza kuwa mpango uliowekwa leo saa saba ni kuzindua Website ya timu ambayo itatanua uwanda wa sehemu za kutolea taarifa.
“Unajua kwa sasa Simba ina mkakati wa kuboresha vyanzo vya kutoa taarifa hivyo imeamua kuanzisha Website ya timu ambayo itakuwa rasmi na itazinduliwa majira ya saa saba na wameletwa wataalamu wengi wa masuala ya mitandao,” ilieleza taarifa hiyo.
Championi Jumamosi lilimtafuta Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu ambaye alisema kuwa hajatambua ni nini ambacho kitafanyika saa saba kwa kuwa hawajakaa kikao
Post a Comment