UONGOZI wa Yanga umesema kuwa wachezaji wanafurahi kuwa kambini kwa sasa huku malengo makubwa yakiwa ni kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zilizobaki.
Yanga imeshaanza mazoezi tangu Mei 27 baada ya wachezaji kuanza kuripoti kambini na kufanyiwa vipimo vya afya.
Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona na tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza ifikapo Juni Mosi.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema:" Wachezaji wapo sawa na kila mmoja anafurahi kuwa kambini, malengo yetu ni kuona tunapata matokeo chanya kwenye mechi zetu zilizobaki,".
Yanga imecheza mechi 27 za ligi kibindoni ina pointi 51 na imefunga mabao 31ambapo katika mabao hayo kiungo wao Bernard Morrison amefunga mabao matatu na kutoa pasi tatu za mabao
Post a Comment