KIUNGO wa Simba, Francis Kahata raia wa Kenya amesema kuwa mabosi wake wa sasa wapo vizuri kwenye masuala ya mipango tofauti na Gor Mahia.
Kahata alitua ndani ya Simba akitokea Kenya alipokuwa akikipiga ndani ya Gor Mahia msimu wa 2019/20 kwa sasa yupo nchini Kenya.
Nyota huyo amesema:-"Simba ipo vizuri kwa upande wa mshahara pamoja na ushirikiano ambao unatolewa kuanzia kwa viongozi pamoja na wachezaji ninafurahi kuwa ndani ya Simba."
Kahata ametupia jumla ya mabao manne na kutoa pasi sita za mabao kati ya mabao 63 ya Simba
Post a Comment