UONGOZI wa Simba umesema kuwa nyota wao wote waliowasili kambini jana maeneo wamefanyiwa vipimo vyote muhimu ikiwa ni pamoja na Virusi vya Corona ili kujua hali zao kabla ya kuanza mazoezi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba Patrick Rweyemamu amesema kuwa wameanza mchakato wa kuwapokea wachezaji wao ambao walianza kuwasili kambini jana.

“Utaratibu uliopo kwa sasa ni kwa wachezaji wa ndani kuanza kuripoti kambini na kazi ya kwanza ni kufanyiwa vipimo ikiwa ni pamoja na Corona lengo ni kujua afya zao kabla ya kuanza mazoezi.

“Kila kitu kinakwenda kwa program na jambo la kwanza ilikuwa kuwasili kambini kisha kupimwa na kuwapa maelekezo ya kitaalamu namna ya kujikinga na Corona," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.