MAJEMBE ya kazi mengine ndani ya kikosi cha Simba yanatarajiwa kuripoti kambini leo baada ya wengine kuanza kuripoti jana.
Patrick Rweyemamu, Meneja wa Simba amesema kuwa wachezaji watakaoripoti kambini wote watapimwa afya na kuendelea na program nyingine ambazo zitapangwa.
Baadhi ya nyota wa Simba ambao wamesharipoti kambini hawa hapa:-Aish Manula, Beno Kakolanya, Ally Salim, Jonas Mkude, Pascal Wawa, Gadiel Michael, Shomari Kapombe, Meddie Kagere, Mohamed Hussein, Miraj Athuman.
Said Ndemla, Deo Kanda, Hassan Dilunga, Rashid Juma,Haruna Shamte,Yusuph Mlipili, Kenedy Juma,Tairone Santos, Gerson Fraga, John Bocco, Luis Misqussone na Erasto Nyoni
Post a Comment