TIMU ya Polisi Tanzania inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara tayari imeanza mazoezi kujiaandaa na Ligi Kuu Bara.

Masuala ya michezo yalisimamishwa na Serikali Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Kwa sasa tayari Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza ifikapo Juni Mosi.

Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Frank Lukwaro amesema kuwa nia ya kuanza mazoezi mapema ni kuimarisha kikosi ili ligi itakapoanza wawe tayari kwa mapambano.

Polisi Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu, Malale Hamsini ipo nafasi ya sita ikiwa imecheza mechi 29 kibindoni ina pointi 45

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.