UONGOZI wa Klabu ya Lipuli umewaomba wadau waendelee kuipa sapoti timu hiyo ili iweze kufikia malengo wayojiweka.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ndani ya Klabu ya Lipuli, Wille Chikweo amesema kuwa mafanikio kwenye mashindano yao yanahitaji sapoti kutoka kwa wadau.
"Kwenye kila mashindano ambayo tunashiriki ni muhimu kupewa sapoti kutoka kwa wadau pamoja na mashabiki, imani kubwa ni kuona kwamba kila mmoja anaendelea kuwa bega kwa bega katika mapambano.
"Tunahitaji kuona timu inafikia malengo makubwa kwenye mashindano ambayo tunashiriki ila haiwezi kuwa rahisi iwapo hakutakuwa na sapoti, kwa wadau wetu wote ambao wapo pamoja nasi tunawaambia asante," amesema Chikweo.
Lipuli FC ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo ikiwa na pointi 33 baada ya kucheza mechi 29 ligi ilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Corona inatarajiwa kuanza Juni Mosi ambapo itachezwa kwa vituo
Post a Comment