Majina haya yanayowapasua kichwa mabosi wa Simba, Yanga na Azam FC kuwapata nyota hawa msimu ujao ili kuboresha vikosi vyao.
Inaelezwa kuwa kila mmoja kwa wakati wake anafanya mpango wake ili kupata saini ya mchezaji mmoja iwapo mambo yatatiki basi anaweza kuibuka ndani ya timu moja kati ya hizi tatu msimu ujao
:- Relliants Lusajo mshambuliaji wa Namungo
amewekwa kwenye rada za Yanga na Simba nao wanatajwa kuiwinda saini yake.
Yusuph Mhilu mshambuliaji wa Kagera Sugar jina lake linatajwa pale Jangwani timu yake ya zamani.
Bakari Mwamnyeto beki chipukizi wa Coastal Union anatajwaYanga, Azam na Simba.
Cleophance Mkandala kiungo wa Tanzania Prisons anatajwa kuingia anga za Yanga na Azam FC.
Hassan Kabunda winga wa KMC anatajwa kuingia anga za Yanga na Azam FC.
Daniel Mgore kipa wa Biashara United huyu anatajwa kuingia anga za Azam FC.
Waziri Jr wa Mbao FC anatajwa kuingia anga za Yanga.
Bigirimama Blaise wa Namungo anatajwa pale Jangwani.
Ibrahim Ame wa Coastal Union beki huyu anatajwa pale Msimbazi na Jangwani.
Jonathan Nahimana huyu anatajwa pale Msimbazi.
Lukas Kikoti kiungo wa Namungo jina lake linatajwa Simba huku Yanga pia wakimtazama kwa ukaribu.
Post a Comment