WACHEZAJI wote wa Klabu ya Yanga tayari wameripoti kambini na kuanza kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi zilizobaki za Ligi Kuu Bara.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa ni mchezaji mmoja tu ambaye hayupo kambini kwa sasa kutokana na kukwama nchini Kenya ambapo mipaka imefungwa.
"Wachezaji wote wameripoti kambini isipokuwa Shikalo yeye yupo Kenya, imekuwa ngumu kuripoti kwa sasa kutokana na mipaka ya huko kufungwa kutokana na tahadhari dhidi ya ya Virusi vya Corona ila mambo yakiwa sawa atarudi muda wowote kuanzia sasa," amesema.
Machi 17 masuala ya michezo yalismamishwa na Serikali kutokana na kusambaa kwa kasi kwa Virusi vya Corona jambo lililopeleka wachezaji kupata mapumziko ya lazima
Post a Comment