IMEWEKWA wazi kuwa, asilimia 90 nyota wa Coastal Union, Bakari Mwamnyeto yupo kwenye hatua ya kutua ndani ya Klabu ya Yanga ambayo imeonesha nia ya kupata saini yake.

Kassa Mussa, meneja wa beki huyo amesema mazungumzo na mabosi wa Klabu ya Yanga yamekwenda vizuri.


Meneja huyo aliweka wazi kuwa Yanga iliwekeza nguvu nyingi kupata saini ya beki huyo ili kujiunga ndani ya timu yao licha ya kutakiwa na timu nyingi.


 "Yanga waliwekeza nguvu kubwa ya kumtaka mchezaji wetu na jitihada zao zimezaa matunda kwa maana kwa asilimia 90 kila kitu kimekwenda sawa. 

"Kinachosubiriwa kwa sasa ni msimu kumalizika ili atoke zake hapo alipo aibukie Yanga kwa ambapo tumefika ni ngumu dili lake kushindikana," amesema Kassa.

Beki huyo chipukizi ni tegemeo kikosi cha kwanza pia ni nahodha licha ya kuwa ni beki ametupia bao moja

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.