UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado unaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona ili kujiweka salama kabla ya kuanza kucheza mechi za ushindani.

Masuala ya michezo yalisimamishwa Machi 17 na Serikali kutona na janga la Virusi vya Corona ambalo linaivuruga dunia na kwa sasa Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza Juni Mosi huku tahadhari zikizingatiwa.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wamekuwa wakiwapa elimu wachezaji kuhusu namna ya kujilinda na Corona huku wakiendelea kuchukua tahadhari kujilinda zaidi.

"Wachezaji baada ya kuripoti kambini walifanya vipimo vya afya ili kujua hali zao na pia wamepewa semina kuhusu namna ya kujikinga dhidi ya Corona lengo wawe salama na wafanye kazi kwa umakini," amesema.

Yanga ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi zake 51 kibindoni baada ya kucheza mechi 27

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.