SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ana imani ya kumtumia kiungo wake mshambuliaji Miraj Athuman,'Sheva' kwenye mechi zilizobaki kutokana na kurejea kwenye ubora wake.
Sheva alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha aliyoyapata wakati akiitumikia timu ya Taifa ya Tanzania kwa sasa amesharejea kwenye ubora wake.
Jana Sheva alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao waliripoti kambini na kuanza mazoezi mepesi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Simba uliopo Bunju.
Sven amesema:"Mapumziko ya Virusi vya Corona yamechangia kwake kuweza kutengamaa na kwa sasa yupo vizuri na ninamuona akiwa kwenye ubora wake hivyo itaongeza upana wa kuchagua nani aanze kwenye kikosi."
Sheva ametupia jumla ya mabao sita kati ya 63 yaliyofungwa na Simba na ametoa pasi moja ya bao lililofungwa na Meddie Kagere
Post a Comment