KOCHA Mkuu wa Simba Patrick Aussems, ameonekana kuvutiwa na kasi ya straika wake mpya Mkongomani, Deo Kanda kutokana nauwezo alionao na kudai kuwa msimu unaokuja kazi itakuwa kubwa.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, Aussems alisema, baada ya kuona kasi ya straika huyo kwa kushirikiana na wenzake kama Meddie Kagere na John Bocco, ametoa maagizo mapya ambayo lazima wayatekeleze.

Aussems amewapa mtihani mkubwa mastraika wake baada ya kuwaambia mzunguko wa kwanza utakapomalizika kila mmoja atatakiwa kuwa na mabao yasiyopungua 10.

Wekundu hao wa Msimbazi ambao leo wanarejea kutoka Afrika Kusini walikoweka kambi, ndio walitoa mfungaji bora msimu uliopita ambaye ni Meddie Kagere, aliyepachika jumla ya mabao 23.

Mbali na Kagere, nahodha wa kikosi hicho John Bocco pamoja na Mganda Emmanuel Okwi, kila mmoja alipachika mabao 16 na sasa Aussems amesema msimu huu anataka kitu kikubwa zaidi.

Akizungumza na DIMBA Jumatano, kutoka Afrika ya Kusini Aussems alisema, malengo yake ya msimu huu ni tofauti na msimu uliopita kwani anataka kutetea ubingwa mapema na ikiwezekana bila kupoteza mchezo wowote.

Natambua tuna kazi kubwa lakini ratiba yangu ya mwaka huu nisingependa iingiliane na mambo mengi, zaidi nataka timu yangu ifanye vizuri kwa kila mechi hasa hizi za mzunguko wa kwanza.

Ninataka mastraika wangu kila mmoja afunge sio chini ya mabao 10 katika mzunguko wa kwanza, naamini hilo linawezekana kabisa. Nadhani hiyo inaweza ikawa njia mojawapo ya Simba kufikia malengo yake mapema, hakuna kinachoshindikana kwani kikosi changu ni kipana na kila mchezaji anataka kupata nafasi ya kucheza, alisema.

Mbali na Ligi Kuu, pia Aussems alisema anataka kuiona Simba ikifikia malengo yake ya kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa Afrika kama ilivyokuwa msimu uliopita. Msimu uliopita Simba walitinga hatua ya robo fainali na kutolewa na TP Mazembe ya DR Congo

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.