Aliyewahi kuwa mchezaji wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amesema kuwa kikosi cha timu hiyo juzi kiliingia kucheza na UD Songo wakiwa na matokeo ya msimu uliopita.

Julio amesema kuwa wachezaji wa kikosi hicho waliingia wakijiamini kwa kuichukulia Songo kama timu ya kawaida lakini badala yake ikapelekea kutolewa kwenye mashindano.

Katika mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa, Simba na Songo walimaliza mechi kwa matokeo ya 1-1 yaliyokuwa na faida kwa wapinzani ambao walisalia kwa faida ya bao la ugenini.

Aidha, mbali na kusemea hilo, Julio amesema pia hakuna wachezaji kutoka Brazil wanaoweza kuja Tanzania kwa ajili ya kucheza soka.

Ameeleza kuwa wabrazil watatu waliosajiliwa wamekuja kwa ajili ya upigaji na kutalii na akieleza kuwa kuna watu watakuwa wamekula pesa.

"Hakuna mbrazili anayeweza kuja kucheza soka Tanzania.

"Watu wa huko wana malengo ya kucheza soka la mbele zaidi, hao wamekuja kutalii tu na si wachezaji mpira, subiri mtaona." 

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.