Klabu kongwe ya baseball, New York Yankees (Dola4.6bilioni) ni ya pili na timu ya mpira wa kikapu ya New York Knicks (Dola 4bilioni) inamazliza tano bora, nyuma ya Real (Dola 4.24 bilioni) na Barca (Dola 4.02 bilioni).

LONDON, ENGLAND. Manchester United imeendelea kutelemka katika orodha ya klabu zenye utajiri mkubwa duniani. Jarida la Forbes limeripoti kwamba klabu hiyo sasa imeshika nafasi ya sita kwa utajiri duniani.

Nafasi hiyo ya Manchester inanamaanisha kwamba imeanguka kwa nafasi nne kutoka nafasi ya pili mwaka jana. 

‘The Red Devils’ sasa wapo nyuma ya vinara wa Clasico yaani Real Madrid (ambayo ni ya tatu) na Barcelona (mabayo ni ya nne). Timu hizo za Hispania zimeendelea kushikilia nafasi hizo, ambazo walizipata mwaka jana. 

Klabu nyingine tano za soka ambazo zimo katika orodha ya klabu 50 bora ni Bayern Munich (17), Manchester City (25), Chelsea (32), Arsenal (42) na Liverpool (45).

Klabu ya NFL ya Dallas Cowboys imeendelea kushika nafasi ya kwanza kwa takribani miaka minne. Klabu hiyo ina uatajiri wa Dola 5 bilioni. 

Klabu kongwe ya baseball, New York Yankees (Dola4.6bilioni) ni ya pili na timu ya mpira wa kikapu ya New York Knicks (Dola 4bilioni) inamazliza tano bora, nyuma ya Real (Dola 4.24 bilioni) na Barca (Dola 4.02 bilioni).

Klabu 10 tajiri

1. Dallas Cowboys (Dola 5bilioni)

2. New York Yankees (Dola 4.6bilioni)

3. Real Madrid (Dola 4.24bilioni)

4. Barcelona (Dola 4.02bilioni)

5. New York Knicks (Dola 4bilioni)

6. Manchester United (Dola 3.81bilioni)

7. New England Patriots (Dola 3.8bilioni)

8. Los Angeles Lakers (Dola 3.7bilioni)

9. Golden State Warriors (Dola 3.5bilioni)

10. Los Angeles Dodgers/New York Giants (Dola 3.3bilioni)

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.