ETIENNE Ndayiragije, Kocha Mkuu wa Azam FC amesema kuwa ndani ya kikosi chake kuna tatizo kubwa la lugha kwa wachezaji wake kushindwa kuelewana jambo ambalo linamfanya ashindwe kubadili safu yake ya ulinzi.
Mpaka sasa safu ya ulinzi ya Azam FC ipo chini ya beki Nicholaus Wadada, Bruce Kangwa, Yakub Mohamed na Daniel Amoah, huku mlinda mlango akiwa ni Razack Abarola ambao aliwatumia kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Fasil Kenema na aliwatumia pia kwenye mchezo dhidi ya KMC wa Ligi Kuu Bara.
Kwenye mchezo dhidi ya Fasil Kenema ambao ulikuwa wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika, Azam FC ilishinda kwa mabao 3-1 na ule dhidi ya KMC ilishinda bao 1-0.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ndayiragije amesema kuwa sababu kubwa inayomfanya ashindwe kubadilisha safu ya ulinzi ni Lugha ya Kiingereza ambayo wanaitumia.
“Mabeki wangu wanaitumia lugha ya Kiingereza, nashindwa kuwabadilisha hawa kwa kuwa nikiweka wachezaji wengine hakuna atakayeweza kuelewana na wengine, jambo ambalo linanifanya niwatumie muda wote,” amesema Ndayiragije.
Post a Comment