Mwanaspoti lilipenyezewa habari na mtu wa karibu wa Maka kwamba, kiungo huyo aliachana na dili la Latvia na hivi sasa amekamilisha usajili ndani ya Morocco.

Dar es Salaam.NEEMA ya wachezaji wa Tanzania kwenda kucheza nje ya nchi imezidi kuongezeka, baada ya kiungo wa Yanga, Edward Maka kujiunga na Atheletico De Tetuan inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Morocco.

Maka (19), amejiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka minne akitokea Yanga.

Maka, ambaye alibakiza mkataba wa mwaka mmoja na Yanga, aliondoka mapema mwezi Juni kwenda nchini Latvia kufanya majaribio na klabu ya Spartaks Jurmala, lakini baadaye alirejea kimya kimya na sasa ameibukia Morocco.

Mwanaspoti lilipenyezewa habari na mtu wa karibu wa Maka kwamba, kiungo huyo aliachana na dili la Latvia na hivi sasa amekamilisha usajili ndani ya Morocco.

"Kweli nipo Morocco hivi sasa na mipango imekwenda sawa, Latvia maisha yalikuwa magumu na mlo ulikuwa ni mmoja tu. Nilikomaa na majibu yalikuwa mazuri, lakini walisema uwezo wangu na viungo waliopo klabuni upo sawa hivyo, wakala wangu ndio akanambia nirudi," alisema.

Kuhusu dili la Morocco alisema alikwenda kama kawaida kufanya majaribio na baada ya kucheza mechi nne za kirafiki ndio alipopata nafasi ya kusajiliwa.

"Nimesaini mkataba na ilibidi nije huku kwa sababu Yanga walishanitoa katika mipango yao ya msimu ujao, hivyo ilikuwa lazima nipambane kupata nafasi hapa," alisema.

MWAKALEBELA AFUNGUKA

Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema ni kweli mchezaji huyo amejiunga na Atheletico De Tetuan ya Morocco.

Aliliambia Mwanaspoti kuwa timu hiyo ilituma ofa ndipo wakakubaliana huku kukiwa na kipengele cha kupata pesa pindi mchezaji huyo atakapouzwa baadaye.

"Kweli yupo huko na wakimuuza tutakuwa tunapata asilimia 20, tumewaruhusu na tumewapa barua, lakini hatujamuuza," alisema.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.