OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wa marudio wa kimataifa dhidi ya UD Songo tiketi ziaanza kuuzwa Alhamisi.
Simba itamenyana na UD Songo mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Agosti 25 uwanja wa Taifa baada ya ule wa awali kutoka suluhu nchini Msumbiji.
Mchezo huo utaanza saa 10:00 jioni viingilio vitakuwa mzunguko shilingi 5000, VIP B na C shilingi 15,000, VIP A shilingi 30,000, Platinum shilingi 100,000 na Platinum Plus shilingi 150,000.
Post a Comment