BABA mzazi wa beki wa Yanga, Kelvin Yondani, mzee Patrick Yondani amefunguka kuwa kuelekea msimu mpya hana hofu na kiwango cha kijana wake huyo hata wakikutana na Simba hakuna mshambuliaji ambaye anaweza kumsumbua.

Mzee Patrick amesema kuwa Simba wao msimu huu wamesajili washambuliaji wapya lakini siyo kwamba kijana wake atashindwa kukabiliana nao.

Katika safu ya ushambuliaji, Simba imesajili wachezaji kama Deo Kanda, Wilker Henrique, Francis Kahata wakiungana na wale wa zamani ambao ni Meddie Kagere na John Bocco.

Mzee Yondani alisema kuwa beki huyo amekuwa kwenye kiwango bora kwa muda mrefu ndiyo maana amekuwa hatetereki uwanjani. Amesema ubora wa kijana wake unazidi kuimarika kadiri muda unavyozidi kwenda na pia amekuwa akizingatia yale ambayo anaelekezwa.

“Ni kweli kijana wangu Kelvin akiwa uwanjani ni mzuri na hilo wengi wanalijua, hakuna fowadi ambaye anaweza kumshinda sababu amekuwa na uwezo wa kuwasoma mapema kabla ya wao hawajamsoma na hicho ndicho kinamfanya kuwa bora.

“Hata kama wakicheza na Simba leo hii, hakuna wa kumtisha, haijalishi wamesajili mchezaji kutoka wapi, kikubwa yeye amekuwa akionyesha ubora ndiyo maana inakuwa rahisi kukabiliana na wapinzani wake.

“Nafurahia kuona kadiri muda unavyokwenda ndiyo anazidi kuitendea haki nafasi yake, nitazidi kumuombea afike mbali zaidi,” alisema mzee Yondani.
Tags: ,

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.