SIMBA na Azam usiku wa leo Jumamosi watavaana kwenye mechi ya Ngao ya Jamii, huku kila timu ikitamba kubeba ngao ya msimu huu.
Hakuna anayejua ni timu ipi itanyakua taji kwenye mechi ya leo ikiwani ni ya 12 tangu kuasisiwa kwa michuano hiyo.
Hata hivyo, hapa chini ni orodha ya mechi 11 zilizopigwa na kutoa washindi tangu michuano hiyo ilipoasisiwa mwaka 2001 na kusimama kisha kuendelea tena 2009.
Mechi za Ngao ya Jamii tangu 2001
2001- Yanga 2-1 Simba
2009- Mtibwa 1-0 Yanga
2010- Yanga 0-0 (3-1pen) Simba
2011- Simba 2-0 Yanga
2012- Simba 3-2 Azam FC
2013- Yanga 1-0 Azam FC
2014- Yanga 3-0 Azam FC
2015- Yanga 0-0 (8-7 pen) Azam FC
2016- Azam FC 2-2 (4-1 pen) Yanga
2017- Simba 0-0 (5-4 pen) Yanga
2018- Simba 2-1 Mtibwa
2019- Azam v Simba ???
Post a Comment