Na Shabani Rapwi


Klabu ya Bayern Munich imethibitisha kukamilisha usajili wa kiungo Philiphe Countinho kutoka Barcelona kwa mkataba wa mkopo wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kumnunua moja kwa moja mwishoni mwa msimu.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 alijiunga na Barcelona Januari 2018 akitokea klabu ya Liverpool kwa dau la Euro Milioni 160 na ilisaini mkataba wa miaka mitano na nusu.

Akiwa Liverpool, Coutinho alicheza mechi 201 na kufunga magoli 54 na alijiunga na Liverpool, Januari 2013 akitokea Inter Milani kwa dau la Euro Milioni 8.5.

Msimu uliopita, katika msimu wake wa kwanza akiwa na Barcelona, Coutinho alicheza mechi 54 za mashindano yote akifunga magoli 11 na kutoa pasi ya mwisho (Assist) tano.

Coutinho ametwaa makombe manne akiwa ndani ya Barcelona, La Liga (2017-18), (2018-19), Copa del Rey (2017-18) na Supercopa de España (2018).

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.