HARUNA Niyonzima, nyota wa zamani wa Simba na Yanga anayekipiga AS Kigali atakuwa na kibarua kizito Ijumaa, mbele ya KMC mchezo wa marudio wa kombe la Shirikisho uwanja wa Taifa.

Tayari uongozi wa KMC umetangaza viingilio kwa ajili ya mchezo huo wa marudio huku kwa buku mbili tu shabiki ataona namna Niyonzima atakavyopata taabu Vitalis Mayanga wa KMC.


Anuary Binde, Ofisa Habari wa KMC amesema wameweka viingilio rafiki ili mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa sapoti timu. 

"Tumeamua kuweka viingilio vidogo ili kuwafanya watu wengi waje uwanjani kutusapoti. Mzunguko itakuwa shilingi 2000 na VIP shilingi 5000 lengo letu ni kupata idadi kubwa ya mashabiki," amesema Binde.
Mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Rwanda KMC ililazimisha suluhu ya bila kufungana ina kibarua kufanya kweli nyumbani.


Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.