Barcelona imefutilia mbali uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wao wa zamani Neymar, 27, kutoka Paris St-Germain katika dirisha hili la usajili. (Goal.com)

Manchester United wameafikiana kwa mkataba wa usajili wa mwaka mmoja wenye thamani ya pauni milioni 6.2 na mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, 33.

Nyota huyo wa kimataifa wa Croatia huenda pia akafikia gharama ya karibu £15m au atakuwa sehemu ya makubaliano ya kubadilishana na mshambuliaji wa United na Ubelgiji, Romelu Lukaku, 26. (Mail)


Romelu Lukaku aliifungia United Mabao 15 msimu uliyopita

Real Madrid wameamua kumsajili mchezaji wa safu ya kati wa Ajax, Mholanzi Donny van de Beek, 22, badala ya kung’ang’ania usajili wa Mfaransa Paul Pogba, 26 kutoka Manchester United. (Marca)

Leicester inatathmini uwezekano wa kumsajili James Tarkowski, 26, wa Burnley ama Nathan Ake, 24, wa Bournemouth katika safu yao ya ulinzi kuchukua nafasi ya beki wao Muingereza Harry Maguire, 26, ambaye anahusishwa na harakati za kuhamia Man Uni..

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.