KIUNGO mpya wa Simba, Ibrahim Ajibu ambaye amejiunga na kikosi hicho akitokea Yanga kwa kandarasi ya miaka miwili, anateswa na rekodi yake aliyoiweka msimu uliopita akiwa na Yanga.
Ajib alihusika kwenye mabao 23 ndani ya Yanga ambayo ilifunga jumla ya mabao 56 na kumaliza Ligi Kuu Bara ikiwa nafasi ya pili ikiwa na jumla ya pointi 86.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Ajibu alisema kuwa kwa sasa hakuna kinachomuumiza kichwa zaidi ya kufikiria namna atakavyofanya vema kwenye kikosi chake kipya na kuweka rekodi nyingine.
“Siku zote mchezaji anafikiria kufanya vizuri ndani ya timu hicho ndicho ambacho nami pia nafikiria, msimu uliopita nilipambana na kuonekana hivyo msimu mpya pia nina jukumu la kufanya kwa ajili ya timu.
“Uwepo wangu ndani ya Simba ni mipango yangu mwenyewe na kwenye suala la kuanza ama kutokuanza hilo mimi sijui zaidi ya kocha, lakini kikubwa ambacho ninafikiria ni kufanya vizuri kwa ajili ya timu, alisema Ajibu.
Post a Comment