Sanchez uhusiano wake na wachezaji na wafanyakazi wengine wa Man United uliingia kwenye mushkeli baada ya kufichuka kuwa analipwa mshahara wa Pauni 505,000 kwa wiki.

MILAN, ITALIA. ALEXIS Sanchez ameripotiwa kwamba kwa muda wote aliokuwa Manchester United alijitenga na wachezaji wengine wote kwenye timu hiyo isipukuwa Romelu Lukaku tu, ndiye aliyekuwa swahiba wake na kupanga mambo pamoja.

Staa huyo wa Chile ameamua kuachana na Man United akienda kujiunga na Inter Milan kwa mkopo, huku atakwenda kukutana na swahiba wake, Lukaku, ambaye amejiunga pia na timu hiyo kwenye dirisha hili la majira ya kiangazi huko Ulaya kwa ada ya Pauni 73 milioni.

Kwa mujibu wa The Athletic, taarifa za kutoka ndani ya Man United, zinafichua kwamba Sanchez alikuwa akizungumza na Lukaku tu na aliwachunia wachezaji wengine wote huko Old Trafford.

Kiwango cha staa huyo kimekuwa cha hovyo tangu alipotua Man United akitokea Arsenal Januari 2018, huku ubora wake ukishuka siku hadi siku na hali ilikuwa mbaya baada ya kufika hadharani mshahara wake anaolipwa kwa wiki. Taarifa nyingine zimedai hiyo ni kawaida kwa Sanchez, kwani hata Arsenal hakuwa na marafiki.

"Alikuwa aina ya wale wachezaji kama tumeshinda 1-0 na yeye hajafunga, basi akiingia vyumbani anapiga vitu mateke. Kama akifunga mabao mawili, lakini tumefungwa mechi, yeye kwake ni sawa. Hakuwa akijichanganya na wachezaji wenzake. Ni mara chache sana," ilifichua taarifa hiyo.

Sanchez uhusiano wake na wachezaji na wafanyakazi wengine wa Man United uliingia kwenye mushkeli baada ya kufichuka kuwa analipwa mshahara wa Pauni 505,000 kwa wiki. Mshahara huo ulianza kuvuruga hali ya hewa kwenye timu, ambapo Paul Pogba akitaka kulipwa mkwanja mrefu, ambapo wakala wake Mino Raiola alianza kuleta habari za kutaka kuondoa pengo hilo la tofauti ya mshahara.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.