Ligi Kuu Tanzania Bara imeshaanza kutimua vumbi mabingwa watetezi ambao ni Simba wanaanza rasmi kazi yao Agosti 29 kwa kuanza kazi mbele ya JKT Tanzania.

Kazi kubwa ambayo wanayo ni kutetea kombe lao walilonalo mkononi huku ushindani ukitajwa kuwa mkubwa kutokana na timu nyingi kujipanga.

Miongoni mwa nyota wapya ambao wamesajiliwa msimu huu na kushtua kidogo ndani ya Simba ni aliyekuwa nahodha wa Yanga Ibrahim Ajibu ambaye amesaini kandarasi ya miaka miwili.

Uwezo wake kwa msimu wa mwaka 2018-19 anashikilia rekodi ya kutoa pasi nyingi za mabao akiwa amefanya hivyo mara 17 na alifunga mabao 6.

Hesabu zake kwa sasa ndani ya klabu yake mpya zipo namna hii:-

Kwa nini Simba?

“Hakuna mchezaji anayeweza kuchagua kambi, nilikuwa Simba awali kabla ya kuibukia Yanga na sasa nimerejea Simba hakuna tatizo lolote.

“Kikubwa ni kubaki kwenye maisha yangu ya soka na kuendelea kucheza soka kwani maisha lazima yaendelee siku zote.

Dili la TP Mazembe limeishaje?

“Nilizungumza nao awali nikaona dili lao ni la kawaida, hivyo haikuwa na ulazima mimi kusaini sehemu ambayo sina maslahi mazuri.

“Nilitazama dili la Simba nikagundua kwamba lipo vizuri nikaamua kusaini hivyo wakati mwingine tutajua yatakayotokea mbele.

Ushindani wa namba?

“Hauwezi kufikiria ushindani wa namba kwa sasa, hakuna sehemu ambayo hakuna ushidani wa namba kila timu hilo lipo hata kule nilikokuwa kulikuwa na ushindani na ndio maana kuna wakati nilianza benchi ama nilipokuwa sipo sawa kuna wachezaji walicheza.

“Sina hofu na benchi kwani kazi ya kupanga kikosi ni ya kocha yeye ndiye anayeamua nani aanze na nani akae benchi, jitihada na kujituma ndicho ninachofikiria.

Mipango ndani ya Simba?

“Siwezi kufanya mipango peke yangu ni lazima nishirikiane na wachezaji wenzagu, wakati huu tunaamini tutakuwa bora na tutafanya mambo makubwa.

“Kitu kikubwa ambacho mashabiki wanahitaji ni matokeo hivyo tutafanya kazi kubwa kupata matokeo chanya wakati wa ligi na mashindano mengine.

Mashabiki wa Yanga unawaambia nini?

“Maisha ya mpira yanabadilika, mchezaji kuhama ni jambo la kawaida kwa kuwa ni kazi yake, walikuwa nasi bega kwa bega na walitupa sapoti nami ninawashukuru kwa hilo.

“Kwa sasa nipo sehemu nyingine haina maana kwamba tunakuwa maadui bado sisi ni marafiki na shabiki atabaki kuwa shabiki hivyo wasikasirike katika hili haya ni maisha.

Rekodi yako je?

“Hicho ni kitu ambacho kipo kwenye mipango, kila baada ya siku kuanza hesabu zangu ni kuona kwamba ninafanya vema kwa manufaa ya timu na Taifa kiujumla hivyo muda upo na rekodi zimewekwa ili zivunjwe.

Kipi kitakupa ushindi?
“Sishindani peke yangu, ushirikiano ambao utakuwa ndani ya timu ndio utakaotupatia mafanikio na ushindi kwenye mashindano yetu ambayo tutashiriki.

Mashabiki wa Simba unawaambia nini?

“Haraka haraka haina baraka walisema, hivyo ni muda wao wa kutulia wenyewe watanipenda kwani ninaamini tutafanya mengi makubwa.

“Simba ni timu kubwa na ina wachezaji wengi wakubwa na kitakachotokea kitakuwa kikubwa mashabiki wasiwe na hofu.

Usajili uliofanywa je unauzungumziaje?

“wote wanastahili ndio maana wamesajiliwa, wengi nilikuwa nafanya nao kazi na wengine wametoka sehemu nyingine ila tofauti zote zinawekwa pembeni na kikubwa ni kazi,” anamalizia Ajibu.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.