Klabu ya Uturuki ya Fenerbahce inataka kumsaini beki wa Manchester United na Argentine Marcos Rojo, 29, kwa mkopo . (A Spor, via Manchester Evening News)
Borussia Dortmund imeongeza maradufu mshahara wa kinda wa miaka 19 wa England Jadon Sancho hadi £80,000 kwa wiki ili kuzuia klabu nyengine kumwania. (Bild - in German)
Klabu za ligi ya Premia Manchester City, Tottenham na Arsenal zinamchunguza kinda wa Renne mwenye umri wa miaka 16 Eduardo Camavinga ambaye aliiongoza klabu hiyo kuilaza PSG 2-1 katika ligi ya daraja la kwanza Ufaransa siku ya Jumapili. (Mail)
Mchezaji mpya wa Real Madrid Real Luka Jovic huenda akajiunga na AC Milan kwa mkopo miezi miwili tu baada ya mshambuliaji huyo ,mwenye umri wa miaka 21 kukamilisha uhamisho wa dau la £62m kuelekea katika klabu hiyo ya Uhispania. (Gazzetta, via Sport Bible)
Monaco imekubali kumsaini kiungo wa kati wa Gabon na Southamptoon Mario Lemina 25 kwa mkoipo wa muda mrefu huku ikiwa na fursa ya kumnunua kabisa.. (RMC - in French)
Liverpool imekataa mwenendo wa klabu ya Denmark Nordsjaelland kumchukua mshambuliaji Bobby Duncan, 20, kwa mkopo wa muda mrefu. (Mail)
Besiktas imekubali makubaliano ya muda mrefu na klabu ya Tottenham kuhusu winga wa Ufaransa Georges Kevin N'koudou. (TRT Spor - in Turkish)
Klabu ya Ubelgiji ya Bruges inataka kumsaini kiungo wa kati wa Tottenham raia wa Kenya Victor Wanyama, 28. (Express)
Post a Comment