Mu Afrika, Sadio Mane anayechezea timu ya Uingereza ya Liverpool, ameorodheshwa kama mojawapo ya wachezaji wenye thamani ya juu zaidi dunia, kulingana na jarida la Football Observator.


Kulingana na jarida hilo, nahodha huyo wa Senagal, almaarufu simba wa Teranga, timu yeyote itakayo taka huduma zake italazimika kutoa kitita cha pauni milioni 144.

Mane ambaye ameorodheshwa nambari sita, amewapiku kina Harry Kane wa Spurs (143M), mwenzake wa Liverpool, Roberto Firmino (132M), Antoine Griezmann wa Barcelona (131M) na kiungo wa Manchester City (125M) katika orodha ya wachezaji kumi waliyo na thamani ya juu zaidi duniani.

Hata hivyo, Mohammed Salah wa Misri ambaye pia anachezea Liverpool ameshangaza wengi baada ya kuwa wa pili katika orodha hiyo huku akiwa na thamani ya millioni 200.

Miongozi mwa wachezaji wanao ongoza orodha la kumi bora ni Kylian Mbappe wa Paris St. Germain (230M), Raheem Sterling wa Manchester City (190M) na Lionel Messi wa Barcelona (153M)

Wachezaji 10 wenye thamani ya juu zaidi

1. Kylian Mbappe (PSG) £230m

2. Mohamed Salah (Liverpool) £200m

3. Raheem Sterling (Man City) £190m

4. Lionel Messi (Barcelona) £153m

5. Jadon Sancho (B. Dortmund) £145m

6. Sadio Mane (Liverpool) £144m

7. Harry Kane (Tottenham) £143m

8. Roberto Firmino (Liverpool) £132m

9. A. Griezmann (Barcelona) £131m

10. Leroy Sane (Man City) £125m

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.