KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa kikosi chake msimu huu hakijaingia kwenye ligi kubahatisha bali ni mwendo wa kichapo kwa kila timu watakayokutana nayo.
Kagera Sugar imefungua duru la ligi kuu kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United ikiwa ugenini kazi yake inayofuata ni mbele ya Alliance FC ambayo imemtimua Kocha wake Athuman Bilal.
Akizungumza na Saleh Jembe, Maxime amesema kuwa funzo walilolipata msimu uliopita limewapa akili jambo linalowapa morali ya kupambana.
“Hatukuwa na matokeo bora msimu uliopita hilo ni darasa kwetu na kwa sasa tunapambana kupata pointi tatu muhimu kwenye kila mchezo kwani hatujaja kutalii.
“Ushindani ni mkubwa nasi tunajipanga kipekee na tutakuwa na mbinu nyingi katika kila mchezo mpya, mashabiki waendelee kutupa sapoti kwani kazi ndio inaanza,” amesema Maxime.
Post a Comment