Zambia haina kocha mkuu wa timu yao ya taifa ya soka 'Chipolopolo' kwa miezi sita sasa tangu ilipoachana na Mbelgiji Sven Vandenbroeck mwezi Februari

Dar es Salaam. Wakati Chama cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ) kikijipanga kumtangaza Kocha Mkuu mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo 'Chipolopolo' wiki hii, kocha wa zamani wa Simba, Pierre Lechantre ni miongoni mwa majina manne yaliyoingia kwenye kinyang'anyiro cha mwisho cha kuwania nafasi hiyo.

Lechantre ambaye aliiongoza Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2017/2018, anawania nafasi hiyo sambamba na makocha Tomislav Ivković, Vaselin Jelusic na Luc Eymael

Hata hivyo Lechantre ambaye ni raia wa Ufaransa anaonekana ana na nafasi finyu ya kuibuka mshindi wa kinyang'anyiro hicho na nafasi kubwa inaonekana kwenda kwa kocha Raia wa Serbia, Vaselin Jelusic.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na gazeti la The Times of Zambia, uongozi wa FAZ tayari umeshamalizana na kocha Jelusic tayari kwa kuinoa timu hiyo.

Uwepo wa mkataba wa ushirikiano baina ya FAZ na Shirikisho la Mpira wa miguu Serbia, unatajwa kama sababu kubwa iliyombeba Jelusic ambaye amewahi kuzinoa timu za Taifa za Angola na Botswana na pia klabu ya Bloemfontein Celtic ya Afrika Kusini.

Kocha wa zamani wa Zambia, Sven Vandenbroeck kutoka Ubelgiji, aliachana na timu hiyo mwezi Februari baada ya kushindwa kuiongoza kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) zilizofanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.