Na Shabani Rapwi
Klabu ya Chelsea wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Stamford Bridge wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Leicester City.

Bao la The Blues limefungwa na Mason Mount dakika ya 7′ kabla ya Wilifried Ndidi kuisawazishia Leicester City dakika ya 67′.

Baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa The Blus, Frank Lampard amesema mchezo ulikuwa mzuri sana asa dakika 25 za kipindi cha kwanza walicheza vizuri licha ya kupoteza nafasi kadha ambazo kama wangezitumia vizuri wangeweza kuzigeuza magoli huku akiwataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa wavumilivu.
“Tulicheza vizuri, na vile ndivyo nilitaka tucheze. Lakini baada ya hapo tukashindwa kumiliki mpira tena. Tulipata nafasi tatu ambazo tungeweza kuzifanya ziwe magoli”.
“Hii ni aina ya mfumo, inatakiwa tuwe na subira na uvumilivu kabla ya kufikia mafanikio”.
MoMchezo huo ni wa pili kwa The Blues katika msimu huu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya wakwanza kufungwa mabao 4-0 na Manchester United katika uwanja wa Old Trafford.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.