KUELEKEA kwenye mchezo wa leo wa ngao ya jamii kati ya Simba na Azam mambo yamezidi kupamba moto ambapo jana Uongozi wa Azam FC ulikuwa na kikao kifupi na wachezaji wa timu hiyo.

Kikao hicho maalumu kilihudhuriwa na viongozi wakubwa ndani ya Azam FC ikiwa ni pamoja na Makamu Mwenyekiti, Omary Kuwe, Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat' na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Azam FC, Nassor Idrissa 'Father' imeelezwa kuwa lengo ilikuwa ni kuwapa nasaha wachezaji.

Habari zinaeleza kuwa lengo kubwa la kikao hicho ilikuwa ni kuwapa morali wachezaji ili warejee na taji la ngao ya jamii kwenye makao makuu ya klabu hiyo maeneo ya Chamazi.

Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa wanaamini mchezo utakuwa mgumu ila wapo tayari kwa ajili ya ushindani licha ya kuwakosa nyota wao wawili ambao ni Mudhathir Yahya na Agrey Morris.
Tags: ,

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.