NA ZAINAB IDDY


BEKImpya waYangaLamine Moro , amesema msimu ujao unaweza kuwa mgumu kwa mshambuliaji wa Simba, Medder Kagere, iwapo  atapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Jangwani.

Moro ambaye ni raia wa Ghana, aliwahi kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa Simba na kuishia kuchezea katika michuano ya Sports Pesa, lakini hakufanikiwa kusajiliwa kabla ya Yanga kumsainisha mkataba wa miaka miwili katika dirisha hili la msimu ujao.

 Akizungumza na BINGWA jana, Moro alisema anamfahamu Kagere, baada ya kukutana naye alipokuja kufanya majaribio Simba, hivyo atahakikisha anamzima.

“Washambuliaji waliopo Simba , Kagere hawezi kunisumbua kwa sababu namjua nilikuwa anaye kipindi nilipokuja kwenye majaribio, nakwambia kama nitapata nafasi hatoweza kupita mbele yangu,”alisema beki huyo.

Wakati huo huo, Moro ameuomba uongozi wa Yanga kumpa jezi yenye namba 25 ambayo pia alikuwa akiitumia pia nchini kwao Ghana.

“Nimeomba jezi namba 25, naipenda hii namba kwa sababu inavitu vingi vilivyobeba maisha yangu, bila shaka ombi langu litakubaliwa,”alisema Moro

Jezi hiyo mara ya mwisho ilikuwa inatumia na beki Hassan Ramadhan ‘Kessy’ ambaye kwa sasa anaichezea  Nkana Red Devils inayoshiriki Ligi Kuu ya Zambia.

Tags: ,

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.