Ukiachana na Kagere, Gadiel amemchambua kiungo mpya wa Simba, Sharaf Eldin Shiboub, raia wa Sudan kwamba anaiona taswira ya jamaa huyu kuupiga mwingi msimu ujao.




GADIEL Michael akiwa Yanga alikuwa na hamu ya kujua siri iliyojificha nyuma ya uwezo wa Meddie Kagere, lakini baada ya kujiunga na Simba amestajabishwa na maisha ya staa huyo na kukiri amejifunza mengi anayoamini atakuja kufanya maajabu kwenye soka.


Aliliambia Mwanaspoti kwamba Kagere alikuwa anamuumiza akili namna ya kumkaba akiwa Yanga, huku akiweka wazi kwamba anajiona mwenye bahati baada ya msimu ujao kucheza naye timu moja, akidai inampa urahisi wa kumsoma zaidi staa huyo.


Alisema Kagere ni kati ya wachezaji ambao alikuwa anapenda aina ya uchezaji wao kwenye Ligi Kuu Bara, akitaja sifa zake kwamba hakati tamaa, mpambanaji, yupo fiti na ana mbinu za kucheka na nyavu kwa nyakati tofauti.


“Nilipokuwa kambini Afrika Kusini, nilikuwa namchunguza Kagere kujua kitu ambacho kinampa mafanikio ya hali ya juu uwanjani, nimebaini ni mtu anayeheshimu kazi yake, anajituma zaidi ya kile anachoelekezwa na kocha.


“Amenifungua macho kwa mambo mengi, najiona nina hatua kubwa ya kiufundi, mchezaji unamuona ana mipango mikubwa ya kufanya kitu kwenye msimu mpya, kifupi nashindwa kumuelezea namna alivyo Kagere na ukweli ni mtu ambaye unaweza ukajifunza vitu kwake.


Amesema, “kila njia ninayotaka kupita ili niweze kuwa na kasi kama yeye tayari alishazipita kitambo na yupo levo nyingine, hayo ndio maisha ya mpira kujifunza sio dhambi, bali inakufanya uwe na hatua na vitu vipya kila unapocheza.”


ALIVYOMUONA MSUDANI


Ukiachana na Kagere, Gadiel amemchambua kiungo mpya wa Simba, Sharaf Eldin Shiboub, raia wa Sudan kwamba anaiona taswira ya jamaa huyu kuupiga mwingi msimu ujao.


“Asikuambie mtu, mchezaji mzuri anajulikana mapema, jamaa pia ni mtu wa kazi, anajituma, ana vitu vingi na adimu vya kimpira, kifupi Simba ina wachezaji wengi wenye viwango vya juu ambavyo vitaleta ushindani mkubwa msimu unaokuja,” alisema.


Mbali na hilo alizungumzia maisha mapya ndani ya kikosi hicho, kwamba awali alikuwa anaona ni tofauti na ilivyokuwa Yanga, akidai kwa sasa ameishayazoea na kujifunza vitu vipya vya kumsaidia kwenye maendeleo yake ya soka.


“Kila sehemu kuna utaratibu wake na mbinu zao kiufundi, mpaka sasa nina hatua kubwa baada ya kujifunza mambo mapya, naamini ipo siku nitakuwa mchezaji wa anga nyingine ndani na nje ya nchi,” alisema.


Tags: ,

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.