NYOTA watano leo watakosekana uwanja wa Taifa ambapo wanaume 22, Simba na Yanga watakuwa wanamenyana kutafuta mshindi wa ngao ya jamii.
Ngao ya jamii ambayo huwakutanisha mabingwa wawili tofauti msimu huu itawakutanisha matajiri wa Dar es Salaam, Azam FC na vigogo Simba.
Jumla ya wachezaji watano kwa timu zote mbili wataukosa mchezo huu kutokana na kusumbuliwa na majeruhi.
Kutoka Simba ni Ibrahim Ajibu, Aish Manula na Wilker da Silver huku kwa upande wa Azam FC ikiwa ni pamoja na Agrey Moris na Mudathir Yahya.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa anatambua ugumu wa mchezo wa leo ila watapambana kupata matokeo chanya.
Kwa upande wa Kocha Mkuu wa Azam FC, Ettiene Ndayiragije amesema kuwa watautumia mchezo wa leo kuandaa kikosi cha kimataifa kitakaochowamaliza Fasil Kenema ya Ethiopia.
Post a Comment