KIUNGO wa Yanga, Abdulaziz Makame, amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo, baada ya kusema kuwa watapambana kuhakikisha wanaibuka na ushindi dhidi ya Township Rollers katika mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA jana, Makame alisema wacheza kwa nguvu zote ili waweze kupata ushindi.
Makame alisema malengo yao ni kufanya vizuri ili kujitengenezea mazingira ya kusonga mbele katika michuano hiyo.
Makame alisema anafahamu kuwa mchezo huo ni mgumu kwa sababu ni wakimataifa, lakini wanahitaji kupambana ili kupata matokeo mazuri.
“Tunajua tuna kazi ngumu,mimi kama mchezaji, ninawaahidi Wanayanga kuwa tutapambana siku ya Jumamosi, mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kutusapoti,” alisema.
Akizungumzia mchezo wao dhidi ya Mlandege, Makame alisema amefurahi kucheza akiwa katika ardhi ya nyumbani kwao Zanzibar na kupata ushindi.
Makame alisema furaha yake inatokana pia kukosa mchezao wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Kariobang Sharks ya Kenya uliochezwa katika kilele cha Wiki ya Wananchi, uliochezwa Jamapili iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa.
Kiungo huyo, hakuwamo kwenye kikosi kilichocheza na Kariobang kwa kuwa alikuwa katika majukumu ya timu Taifa Stars.
Katika hatua nyingine, kiungo wa timu hiyo, Mrisho Ngassa, amesema wanadeni kubwa kwa kocha wao Mwinyi Zahera kuhakikisha wanaifunga Township Rollers.
Yanga inatarajia kukutana na timu hiyo,baada ya mwaka juzi kutolewa katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1. Katika mchezo wa kwanza uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Yanga walifungwa mabao 2-1 na waliporudiana ugenini walitoka sare ya kutofungana.
Post a Comment