TIMA SIKILO


MCHAMBUZI wa soka nchini, Alex Kashasha, amesema benchi la ufundi la Simba limelamba dume katika usajili waliofanya, hasa kwa kuwanasa Sharaf Shiboub na Deo Kanda.

Akizungumza na BINGWA juzi, Kashasha alisema kwa jinsi alivyokiona kikosi cha Simba, kipo kamili kwani hata pengo la wachezaji nyota walioachwa, halionekani.

Alisema pamoja na wachezaji kutozoeana, lakini wanacheza mpira unaoeleweka katika dakika zote ambazo wanakuwa uwanjani.

“Kama hii timu itaendelea hivi kwenye michezo yao yote, kazi itakuwepo katika ligi na hata kwenye hiyo michezo yao ya kimataifa.

“Kulikuwa na malalamiko makubwa kwa kuondoka baadhi ya wachezaji kama Haruna Niyonzima, lakini Sharaf Shiboub anaonekana kuziba pengo lake. Kuhusu Okwi (Emmanuel), kuna Deo Kanda ambaye kwangu mimi huyu ni bora kuliko Okwi,” alisema.

Kashasha ametoa kauli hiyo, ikiwa ni baada ya kuiona Simba ikimenyana na Power Dynamos ya Zambia katika mchezo wa kirafiki jijini Dar es Salaam na ule wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya UD Songo ya Msumbiji uliochezwa ugenini.

Tags:

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.