MAURICIO Pochettino, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Tottenham amesema kuwa Jose Mourinho ni kocha sahihi kubeba mikoba yake ndani ya timu hiyo kwa sasa.
Pochettino alisimamishwa kazi ndani ya kikosi hicho kutokana na mwenendo mbovu wa timu hiyo kwenye Ligi Kuu England kwa sasa imepita miezi sita tangu apigwe chini.
Kwa sasa Pochettino bado hajapata kazi mpya ambapo awali ilikuwa inaelezwa kuwa anaweza kuibukia ndani ya kikosi cha Manchester United ama Real Madrid ili akawe kocha kwenye timu hizo ila mambo hayajawa sawa mpaka sasa.
Raia huyo wa Argentina amesema kuwa bado ana mawasiliano mazuri na Mourinho kwani walikuwa wanatambuana toka muda mrefu imani yake ni kwamba atafikia malengo ambayo aliyaanza kuyafanya hapo awali.
"Amechukua nafasi yangu ndani ya Spurs ninafuraha kuona haya yakitokea nina amini katika uwezo wake yupo vizuri, sikushindwa kufanya kazi ila kuna mambo ambayo yaligoma kwenda sawa," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.