PAPY Tshishimbi, nahodha wa Yanga amesema kuwa yupo tayari kwa ajili ya kupambana ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo ilisimama kutokana na janga la Virusi vya Corona.

Machi 17 Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ilisimamisha masuala ya mikusanyiko isiyo ya lazima ambapo iligusa pia sekta ya michezo.

Mei 21, Rais John Magufuli aliruhusu kuendelea kwa Ligi ambayo inatarajiwa kuanza Juni Mosi na itakuwa kwa mtindo wa vituo ambapo Dar itachezwa Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho huku Mwanza ikichezwa Ligi Daraja la Kwanza na la Pili.

Tshishimbi amesema:" Tuna safari ndefu kufikia mafanikio ila kwa sasa tunaamini mambo yatakwenda sawa na tutakamilisha mechi zetu ambazo zimebaki kwani tulikuwa  tumekosa kucheza kwa muda mrefu."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.