MTENDAJI Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa, amefunguka kuwa wanaendelea kuumiza kichwa juu ya kuwapata wachezaji wao, Francis Kahata na Clatous Chama ambao wapo nje ya nchi kwa ajili ya kumalizia mechi zao zilizobakia za Ligi Kuu Bara.
Senzo amesema kuwa wanaendelea kuwasiliana na wachezaji hao kwa ajili ya kuwarejesha Bongo kuendelea na majukumu yao kwenye kikosi hicho.
Chama, Kahata, Meddie Kagere na Sharaf Shiboub ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wapo kwao baada ya kuondoka mwanzoni mwa mwezi uliopita kwa ajili ya kuzitumikia timu zao za taifa.
Senzo amesema kuwa amekuwa na mawasiliano na wachezaji hao kwa ajili ya kuwarudisha nchini ambapo kwa sasa imekuwa ngumu kwa wachezaji hao kurejea kutokana na mipaka ya nchi hizo kufungwa.
“Tunawasiliana nao wachezaji wote ambao wapo nje na mimi nimekuwa nikiongea nao kila mara kuhusiana na jambo hilo.
“Tunawasiliana nao kuona wanarudi kwa wakati ili waje kumaliza kazi ambazo zimebaki lakini inakuwa ngumu kwa sababu baadhi yao hawawezi kutoka kwani bado ndege haziruhusiwi kutoka kwenda sehemu nyingine,” amesema Senzo
Post a Comment