UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umepokea kwa mikono miwili suala la Ligi Kuu Bara kurejea jambo ambalo wanaamini watapata bingwa kihalali.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona ambalo linaivurugavuruga dunia kwa sasa inatarajiwa kurejea Juni Mosi baada ya Serikali kusema kuwa hali imekuwa shwari.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wana imani mambo yatakwenda sawa huku mipango ikiwa inapangwa kiumakini.

"Kwa sasa nina imani mambo yatakwenda vizuri, tunaamini kwamba bingwa atapatikana kiuhalali uwanjani na mpira tutaucheza kwa umakini.

"Kikubwa ni mashabiki kutupa sapoti na tunatarajia kuanza kazi hivi karibuni kwani tupo tayari na kila kitu kitakwenda sawa," amesema.

Mechi zake zote za Ligi Yanga itachezea Bongo baada ya ligi kusimamishwa kutokana na janga la Corona hivyo mechi zote zitachezwa Dar.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.