PASCAL Wawa beki kisiki wa Simba amesema kuwa hana hesabu za kuleta familia yake Bongo kwa sasa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona.

Machi 17, Ligi Kuu Bara Bara ilisimamishwa na Serikali kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaivurugavuruga dunia ila kwa sasa inatarajiwa kurejea Juni Mosi.


Wawa amesema kuwa mambo bado sio shwari haoni haja ya kuleta familia yake ambayo ipo nchini Ivory Coast. 


"Tunapita kipindi kigumu kwa sasa ila hakuna chaguo la kufanya ni lazima tuombe dua mambo yawe safi, sina mpango wa kuleta familia Tanzania kwa sasa huko walipo tunawasiliana," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.