UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa wameanza michakato ya kuona namna gani watawarejesha wachezaji wao ambao wapo nje ya nchi ili kurejea kuendelea na ligi.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali kutokana na kuibuka kwa janga la Virusi vya Corona ambalo linaivuruga dunia kwa sasa.

Mei 21, Rais wa Tanzania, John Magufuli aliruhusu shughuli za michezo kwa kuwa hali imeanza kutengamaa.

Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingisa amesema:-"Kauli ya Rais tumeisikia kuhusu kurejea kwa ligi mwezi ujao,  nimeshaongea na Meddie Kagere,Clatous Chama,Sharaaf Shiboub na Francis Kahata ambao hawapo nchini kwasasa na tayari mipango ya kuwarejesha haraka inafanyika."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.