KIUNGO wa zamani wa Klabu ya Chelsea, Michael Ballack amesema kuwa ni kweli kwa sasa beki wa Liverpool, Virgil van Dijk yupo kwenye ubora wake ila hakukutana na balaa la kizazi cha Didier Drogba.


Nyota huyo amesema kuwa kikubwa kinachomfanya beki huyo aonekane bora ni pamoja na jitihada zake binafsi za kuzuia mashambulizi Pamoja na kufunga ila aina ya wachezaji anaokutana nao bado haujafikia kizazi kilichopita ndani ya Ligi Kuu England.

Ameongoza kuwa kila mmoja kwa sasa anamuona yeye ni bora kwa kuwa ni wakati wake ila anaamini ingekuwa zama za Drogba angesema yote anayoyajua ndani ya Uwanja.

Dijk mwenye miaka 28 amekuwa ni miongoni mwa mabeki bora ndani ya Ligi Kuu England huku washambuliaji wengi wakimtaja kuwa ni mtu wa kazi ndani ya Uwanja. 


"Ana bahati kwa sasa hajacheza zama zile Ligi Kuu England ikiwa na watu kama Drogba, Lampard (Frank), Alan Shearer, Thiery Henry, Wayne Rooney, Emmanuel Adebayor ni bahati kwake," amesema

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.