TIMU ya KRC Genk anayoichezea nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta leo imefungashiwa virago jumla kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-0 mbele ya Napol.

Mchezo wa leo ulikuwa ni wa ushindani mkubwa ambapo Samatta hakuweza kufurukuta kutokana na kubanwa na mabeki wa timu pinzani ambayo imefuzu hatua ya 16 Bora kwenye michuano hiyo.

Mabao ya ushindi wa Napoli yalipatikana kupitia kwa Arkadiusz Milk ambaye alifunga hat-trick dakika ya 2,26 na 38 kwa penalti huku lile la nne nalo likipachikwa dakika ya 74 kwa mkwaju wa penalti kupitia kwa Dries Mertens.

Genk inayaaga mashindano ikiwa haijashinda mechi hata moja ila Mbwana Samatta anasepa na rekodi ya kufunga mabao matatu kweny michuano hii mikubwa

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.