Kwa mara ya kwanza straika na nahodha wa Simba, John Bocco anarudi uwanjani Januari 4, mwakani dhidi ya Yanga na amewapiga biti kali. Bocco amezikosa mechi 10 za Ligi Kuu Bara kutokana na kuwa majeruhi wa muda mrefu.

Mshambuliaji huyo mwenye rekodi ya kufunga mabao zaidi ya 100 katika ligi atarudi kwenye mechi hiyo itakayopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar.

Bocco tangu amejiunga na Simba misimu miwili nyuma hajawahi kupoteza mbele ya Yanga. Bocco amesema wanajua jukumu lao la kushinda katika mchezo huo ambapo pia wanataka kwa msimu huu kuvunja rekodi ya kufunga mabao matatu katika mechi hiyo ambayo inashikiliwa na Abdallah Kibadeni.

“Tunajua jukumu letu, tutaifunga timu yoyote tupate ubingwa, tutapambana kuchukua pointi tatu katika mechi hiyo dhidi ya wapinzani wetu hao.

“Pia tuna washambuliaji wazuri, sitaki kujitaja mimi, kuna wachezaji wengi na washambuliaji wengi, tutavunja rekodi ya Kibadeni ya kufunga mabao matatu katika mechi ya watani wa jadi."

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.