Uongozi wa Simba umefunguka kuwa tayari watu maalum wanaohusika na masuala ya usajili ndani ya klabu hiyo wameanza kufanyia kazi mapungufu ambayo wamebaini katika kikosi hicho.

Nafasi ambazo Simba inaenda kufanyia kazi kipindi hiki cha usajili ni pamoja na ushambuliaji na
ulinzi.

Katibu wa Simba, Dk Anorld Kashembe alisema masuala ya usajili wapo watu maalum kwa sasa ambao wameanza kufuatilia yale mahitaji ya timu.

“Kuna watu maalum ambao walikuwa wakipewa ripoti zile za kila mchezo na kocha kwamba nini kifanyike kwa hiyo hao watu kwa sasa kuelekea usajili ndiyo watafanya kazi hiyo.

“Wao wanafahamu nini kiongezwe ndani ya Simba na nini kipunguzwe sababu ripoti zote walikuwa wanapata wao. 

“Kocha aliyepo anaendelea na program ya mazoezi kama kawaida kuona kila kitu kinaenda sawa usajili ukiļ¬ ka wahusika wataweka kila kitu wazi,” alisema Kashembe.

Post a Comment

Author Name

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.